JAVIO MADISH PANEL

Monday, November 24, 2014

KIN'GAMUZI CHA BEI POA KULIKO TANZANIA. .......

Ndio ni Startimes tunayofuraha kukupa ndugu mteja punguzo bab kubwa la mpaka 
Tsh 59 ,000/= tu!!! kwa kipindi hiki ya sikukuu za Christmas na mwaka mpya ikiwa na mwezi mmoja wa kuangalia buuure kabisa huku tukikuacha na furaha kwani utafurahia vipindi bomba ndani yake.



Je unangoja nini ni wakati wa kutoka analogia kabisa, bila shaka wamekusema mno kuhusu kutokuwa na kin'gamuzi ila sasa jubu umepata ndugu mteja mtanzania wa kawaida kama mimi. Ofa hii ni kwa ajili ya sikukuu tu!!!! Wahi ni chache.
Bila kusahau pia tunazo anantenna za nje kwa bei nzuri ya Tsh 25, 000/= tu.




Our promotion package include our one month free subscription, one year warranty for decoders.


For enquiry call
+255 714 422729, +255 684 603135.
lhumbahjavio@gmail.com
javiofelix@yahoo.com


                   JAVIO MADISH TUPO KARIBU YAKO!!!!!!!!

Saturday, November 22, 2014

JAVIO MADISH MOB: 0714-422729, 0684-603135: AZAM SERVICE REPAIR

JAVIO MADISH MOB: 0714-422729, 0684-603135: AZAM SERVICE REPAIR: Hebu tizama vyema  picha hii, ukichunguza kwa makini utaona katika kin'gamuzi  hiki hapo mbele kuna taa mbili ndugu mteja, taa hiz...

JAVIO MADISH MOB: 0714-422729, 0684-603135: HII NI KALI ZAIDI, STAR TV KWENYE KIN'GAMUZI CHA A...

JAVIO MADISH MOB: 0714-422729, 0684-603135: HII NI KALI ZAIDI, STAR TV KWENYE KIN'GAMUZI CHA A...: Mabingwa wa madish Afica mashariki na kati tunakuletea channel pendwa ya Star tv iliyo kosekana kwa kipini kirefu kwenye kin'gamuz...

HII NI KALI ZAIDI, STAR TV KWENYE KIN'GAMUZI CHA AZAM



Mabingwa wa madish Afica mashariki na kati tunakuletea channel pendwa ya Star tv iliyo kosekana kwa kipini kirefu kwenye kin'gamuzi chako cha Azam tv. Yapo malalamiko mengi juu ya kukosekana kwa channel hii ila JAVIOMADISH tunakuletea channel hiyo kwa ghalama ndogo tu! Tutaweza kukupatia Star tv na we ukafuraia yaliyomo. Usisite kunitafta kwa maelezo zaidi



For enquiry call
+255 714 422729, +255 684 603135.
lhumbahjavio@gmail.com
javiofelix@yahoo.com
                    
 JAVIO MADISH TUPO KARIBU YAKO!!!!!!!!

AZAM SERVICE REPAIR



Hebu tizama vyema  picha hii, ukichunguza kwa makini utaona katika kin'gamuzi  hiki hapo mbele kuna taa mbili ndugu mteja, taa hizi ama (indicator) kitaalamu ni za  rangi ya njano  na ingine ni ya kijani  taa ya njano inamaanisha (power) maana yake kin'gamuzi kimewaka na hii kwa kawaida huwa inawaka muda wote pindi utakapo washa kin'gamuzi chako, hii kimsingi haina shida. Sasa leo nataka kuongelea taa (indicator)  ya kijani hii kimsingi huusika  na suala zima la signal au mawimbi, hii pia huwaka pindi singnal au mawimbi yanapokua sawa. sasa ushawahi kujiuliza mbona kin'gamuzi chako kina scratch au hakileti picha kabisa kinaonesha ujumbe wa NO SIGNAL???????????.

Jibu ni kwa ndio hapo hakuna mawasiliano kati ya dishi na kin'gamuzi chako na ukiona vitu hivyo basi bila shaka taa ya kijani huwa haitulii hii inakua inacheza cheza kitaalamu tunasema SIGNAL IS LOST.
Ndugu mteja   basi ukiona dalili hizo usisite kunitafuta kupitia namba zangu za simu ama e-mail address zangu nami ntakufikia mara moja kwa marekebisho, ghalama zangu ni chache na utapewa guarantee ya ufundi kwa miezi mitatu tatizo lolote basi ni juu yetu.



For enquiry call
                    +255 714 422729, +255 684 603135.
lhumbahjavio@gmail.
comjaviofelix@yahoo.com?

  JAVIO MADISH TUPO KARIBU YAKO!!!!!!!!

Friday, November 21, 2014

AZAM TV MONTHLY PAYMENTS ON YOUR MOBILE

Je unafahamu kampuni husika kulipia malipo ya mwezi kupitia picha hapo juu

 au mitandao unayoweza kulipia malipo ya mwezi ya AZAM TV hata ukiwa popote pale???? Kumekua na maswali mengi kwa wateja juu ya jinsi ya kulipia malipo ya mwezi, ndugu mteja nipo hapa kukujuza yooote juu ya hili.

MAX MALIPO, SELLCOM, TIGO PESA, M PESA, PAYPOINT
Chukua muda kuzijua kampuni hizo kwa kuangalia picha hapo juu....

 For enquiry call
                    +255 714 422729, +255 684 603135.
lhumbahjavio@gmail.com
javiofelix@yahoo.com

  JAVIO MADISH TUPO KARIBU YAKO!!!!!!!!

AZAM TV BADO INAFANYA VIZURI

AZAM TV




Azam tv bado inaendelea kufanya vyema ususani kwenye nyongezo ya channel, mtu wangu wa nguvu usipate shida je wataka kujua channel zilizopo kwenye kin'gamuzi cha Azam?????? Tafadhali fuatana nami!!!!



MOVIES 
Sinema Zetu 
African Movie Channel
MGM Movie Channel
Star Gold 
Zee Cinema 

 SPORTS
 Vpl/ Azam one Azam two
 Setanta Africa 
Kombat sport 
MCS international

  ENTERTAINMENT
 Azam one 
Azam two 
Wanasah
 E.tv
 Fox entertainment
 Fx
 Star gold
 Euro channel 
Zoom 
Colous 
Mbc 1
 Mbc 4 

KNOWLEDGE
 Nat Geo Gold
 Discovery science
 Investigation discovery

 INTERNATIONAL NEWS
 Al jazeera English 
Al jazeera arabic
 Times now 
Al Arabiya

 MUSIC 
Mtv base
 Mtv India
 Zing
 Box tv

 CHILDREN 
Nickledon
 Al Jazeera kids 

 LIFE STYLE
 Fine living
 Outdoor
 Landscape

 LOCAL
 Itv 
Channel 5
 Channel ten
 Tbc 
Clouds tv
 Zbc
 Bukedde 
Citizen
 Nbs
 K24 
Ntv
 Ktv
 Tv west 
Urban tv 

Bila kusahau hizi channel za local zinadumu kwa muda wa wiki tatu tu baada ya kuisha kifurushi hapo zitaondolewa na kubaki na channel moja tu ya Information channel


+255 714 422729, +255 684 603135.
lhumbahjavio@gmail.com
javiofelix@yahoo.com

Wednesday, November 19, 2014

KAZI SAFI..............NA CONNECTOR

Leo nataka niongelee kitu fulani ni kidogo lakini kina umuhimu mkubwa, tunapoongelea kazi safi hapa kuna mengi ndani yake lakini leo naongelea F-connector, au wengi huita pini.
Kuna hii bahati mbaya huwa inatokea ya waya (cable) inapo hitajika kuungwa au inapokua fupi kwa sababu mbalimbali kifaa hiki hutumika ili kuunga waya ili kuzuia shoti inayoweza hata kuua reciver (kin'gamuzi) chako. Japo kuna mafundi ambapo hawajakamilika wao huunga kienyeji bila kifaa hiki, tambua kua utakua katika hatari ya kuua kin'gamuzi chako lakini muda mwingine mteja kwa kuogopa ghalama za kununua kifaa hiki labda kutokana na udogo wake wa umbo anamuamulu fundi kuunga kienyeji. Jua unakwepa labda elfu tano ila itakuja kukughalimu hata kununua kin'gamuzi kipya.
Tafadhali chukua muda wako kukagua cable yako kama iliungwa je ina kitu kama hiko kwenye picha na kama hakuna kuna tape tu au kumefungwa na mfuko wa nailoni usijali tuwasiliane kwa namba hapo chini nasi tutakufikia kushughulikia ili kunusuru kin'gamuzi chako. Call: 0714 422729, 0684 603135 .

NI KWA UWEZO WA MUNGU TU.......


Tafadhali usiache kusoma hii: LOOK WHERE WE'VE JUST STARTED, unajua mtu alipo lazima kuna mengi kapitia, wapo waliompa moyo na waliomkatisha tamaa, zipo raha na taabu nyingi tu ndani yake. Pasipo juhudi binafsi labda tusingefika hapa, japo wapo watu waajabu sana ndani yake wanaojikuta Miungu watu na kua bila wao eti tusingefika hapa.... hahaha mi nadhani ni ufukara wa kiakili tu kwani mtu anajisahau MUNGU peke yake ndio anapanga hatma ya mtu na kwamba hata wewe umepangiwa tu ipo siku mwenye navyo (Mungu) akihitaji atavichukua ikibidi hata roho yako. Tusijisahau kwa kidogo tulicho nacho, jua kua mali ulionayo ni ubatili mtupu, linda roho yako na si mali. Hujiulizi kuna mtajiri wangapi walikuwepo na sasa hawapo. Kwa kweli ni Mungu peke ndie kawezesha yote hay na si mtu kama mimi au wewe.... Mnakera sana mnaojikuta nyinyi Miungu watu na msemo wenu wa "Bila mimi usingefika ulipo" kubali kataa kama wewe unamawazo ya kijinga hivyo weweni fukara tayari. ONE LOVE

Tuesday, November 11, 2014

MABADILIKO.....STARTIMES YA DISH SOKONI

Naomba niwatoe wasi enyi nyote wapenzi wa Startimes na vipindi vyake sasa wameleta startimes ya dish wametambua hili na kuthamini hili swala la scratch kwenye kin'gamuzi cha antenna .Sasa star sat dish inapatikana kwa Tshs 149, 000/= tu! Ikiwa ni vifaa pamoja na gharama ya ufundi.
Kutokana na kwenda kufa kwa mfumo wa antenna pamoja na malalamiko kuhusu Startimes ya antenna  sasa wameongeza channel pamoja na king'amuzi cha HD picha ya mn'gao na wamemaliza suala la scratch.
Zaidi ya hapo kitu special ni channel za local (za TANZANIA) zinapatikana zote na hata malipo ya mwezi yakikata utabaki na hizi local kwa muda wote wa uhai wako. kazi ni kwako usikose kujipatia. Piga namba zetu 0714 422729, 0684 603135 tukuletee mpaka kwako

Friday, November 7, 2014

CHUNGUZA.....UTAGUNDUA.

Je wakifahamu kifaa hiki kwenye dishi yako?
LNB!!! naam lnb ni kufaa kinacho kaa mbele kwenye mkono wa dish yako kiko mfano wa kikombe kama uonavyo katika picha, sasa leo nataka niwakosoe wale wanaokua mafundi kupitiliza wa kufunika kifaa hiki na makopo au mifuko ya rambo.... nafikiri ni kutofahamu tu, tafadhali usihadaike na kudanganywa na mafundi vishoka kua eti huwa inaharibika ikinyeshewa na mvua au eti mvua ikija basi dishi haikati mawasiliano. Jibu ni NO!!!!!!! tena fundi akikupa ushauri huo hata pesa usimlipe sababu si fundi huyo, kifaa hiki kimetengenezwa kwa ajili ya kukumbana na hali yoyote ya hewa. Mzungu alipounda ilijua kua kuna mvua na kadhalika na kama ni hivyo ange tengeneza cha chuma. Hivyo basi usiingizwe chaka na mafundi wahuni, na kuweka mafuko na makopo ni uchafu tu!.
LNB

Thursday, November 6, 2014

FANTASTIC DUOS.......KILIMA HEWA-TEGETA

Javio nafurahia sana kufanya kazi na huyu jamaa Mustaphamadish kiukweli ni raha sana pale ambapo mteja anaporidhika na kazi, kwakawaida kufunga dishi ni ghalama kiasi chake hivyo basi mteja anapenda au anategemea kazi nzuri na safi tena itayofanana na kiasi cha pesa alicholipa na hili sisi ndilo tunapenda ili kupata credit na kuongeza wateja
Naomba nizungumze nawe ndugu mteja. Tafadhali kamwe usiache kufuatilia blog hii kwan licha ya masuala ya kibiashara lakini pia itakuelimisha sababu madish yamekua ni sehemu ya maisha yetu.
Karibu......

Wednesday, November 5, 2014

OFA! OFA! OFA! BADO INAENDELEA USIPITWE.

Sasa endelea kupata utamu wa show ya kijanja BIG BROTHER AFRICA pamoja na mechi za kukata na shoka kama UEFA CHAMPION LEAGUE, ENGLISH PREMIER LEAGUE na nyinginezo katika kin'gamuzi chako cha digital satellite television (DSTV) bila kusahau MOVIE SERIES za kusisimua kwa ofa ya Tsh 99, 000/= tu!
Pamoja na ghalama za ufungaji....... press ordre na tutakuletea mpaka mlangoni. Piga namba tajwa hapo juu.

JAVIO CREW CAUGHT ON MOVE

Ilipovamiwa Zuku
javio kibaruani.
Leo imekua siku njema kwani huduma imeendelea vilivyo maeneo ya Ubungo kibo ni Zuku sasa twende sambamba sasa.
Twin brah legendary Mustaphamadish on fire....


Usisite kututafuta kwa namba zetu tajwa hapo juu, tupo na hamu ya kukusikiliza na kukuhudumia. Karibu........

Saturday, November 1, 2014

MVUA NA MAWINGU MAZITO

Je hali ya mvua na mawingu yaweza kuleta shida kwenye dish lako?????? Jibu ni kweli, kumekua na malalamiko juu ya dish za makampuni tofauti tofauti hapa kwetu Tanzania na kwengineko.... Je nini tatizo???? Kitaalamu kuna aina mbili za dish KU BAND pamoja na SEA BAND sasa hapa zenye tatizo husika ni KU BAND, KU ambayo kirefu chake ni K- under, hii mara nyingi inatumika kwenye masafa ya rada yanayocheza kwenye 12 - 18 GHz kistandadi ya IEEE 521-2002 na mara nyingi aina hii ya dish hutumika kwa mawasiliano ya kisatelaiti hasa maswala ya broadcast. Mfano wa KU BAND dish ni dish ya AZAM, DSTV, ZUKU, STAR TIMES, TING nk. Nini ufanye mara baada ya kuona tatizo la kukata mawasiliano kwenye TV yako? Usiguse dish wala kufanya setting yoyote mara baada kuona hali hiyo, bali iache Tv pamoja na kin'gamuzi chako mpaka mvua ikipungua basi mawasiliano yatarudi na utafuatilia vipindi uvipendavyo. Ahsante kwa kuchukua muda wako kuelewa hili....