JAVIO MADISH PANEL

Wednesday, November 19, 2014

KAZI SAFI..............NA CONNECTOR

Leo nataka niongelee kitu fulani ni kidogo lakini kina umuhimu mkubwa, tunapoongelea kazi safi hapa kuna mengi ndani yake lakini leo naongelea F-connector, au wengi huita pini.
Kuna hii bahati mbaya huwa inatokea ya waya (cable) inapo hitajika kuungwa au inapokua fupi kwa sababu mbalimbali kifaa hiki hutumika ili kuunga waya ili kuzuia shoti inayoweza hata kuua reciver (kin'gamuzi) chako. Japo kuna mafundi ambapo hawajakamilika wao huunga kienyeji bila kifaa hiki, tambua kua utakua katika hatari ya kuua kin'gamuzi chako lakini muda mwingine mteja kwa kuogopa ghalama za kununua kifaa hiki labda kutokana na udogo wake wa umbo anamuamulu fundi kuunga kienyeji. Jua unakwepa labda elfu tano ila itakuja kukughalimu hata kununua kin'gamuzi kipya.
Tafadhali chukua muda wako kukagua cable yako kama iliungwa je ina kitu kama hiko kwenye picha na kama hakuna kuna tape tu au kumefungwa na mfuko wa nailoni usijali tuwasiliane kwa namba hapo chini nasi tutakufikia kushughulikia ili kunusuru kin'gamuzi chako. Call: 0714 422729, 0684 603135 .

No comments:

Post a Comment