JAVIO MADISH PANEL
Saturday, November 1, 2014
MVUA NA MAWINGU MAZITO
Je hali ya mvua na mawingu yaweza kuleta shida kwenye dish lako??????
Jibu ni kweli, kumekua na malalamiko juu ya dish za makampuni tofauti tofauti hapa kwetu Tanzania na kwengineko....
Je nini tatizo????
Kitaalamu kuna aina mbili za dish KU BAND pamoja na SEA BAND sasa hapa zenye tatizo husika ni KU BAND, KU ambayo kirefu chake ni K- under, hii mara nyingi inatumika kwenye masafa ya rada yanayocheza kwenye 12 - 18 GHz kistandadi ya IEEE 521-2002 na mara nyingi aina hii ya dish hutumika kwa mawasiliano ya kisatelaiti hasa maswala ya broadcast.
Mfano wa KU BAND dish ni dish ya AZAM, DSTV, ZUKU, STAR TIMES, TING nk.
Nini ufanye mara baada ya kuona tatizo la kukata mawasiliano kwenye TV yako?
Usiguse dish wala kufanya setting yoyote mara baada kuona hali hiyo, bali iache Tv pamoja na kin'gamuzi chako mpaka mvua ikipungua basi mawasiliano yatarudi na utafuatilia vipindi uvipendavyo. Ahsante kwa kuchukua muda wako kuelewa hili....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment