JAVIO MADISH PANEL

Friday, November 7, 2014

CHUNGUZA.....UTAGUNDUA.

Je wakifahamu kifaa hiki kwenye dishi yako?
LNB!!! naam lnb ni kufaa kinacho kaa mbele kwenye mkono wa dish yako kiko mfano wa kikombe kama uonavyo katika picha, sasa leo nataka niwakosoe wale wanaokua mafundi kupitiliza wa kufunika kifaa hiki na makopo au mifuko ya rambo.... nafikiri ni kutofahamu tu, tafadhali usihadaike na kudanganywa na mafundi vishoka kua eti huwa inaharibika ikinyeshewa na mvua au eti mvua ikija basi dishi haikati mawasiliano. Jibu ni NO!!!!!!! tena fundi akikupa ushauri huo hata pesa usimlipe sababu si fundi huyo, kifaa hiki kimetengenezwa kwa ajili ya kukumbana na hali yoyote ya hewa. Mzungu alipounda ilijua kua kuna mvua na kadhalika na kama ni hivyo ange tengeneza cha chuma. Hivyo basi usiingizwe chaka na mafundi wahuni, na kuweka mafuko na makopo ni uchafu tu!.
LNB

No comments:

Post a Comment