JAVIO MADISH PANEL

Tuesday, October 28, 2014

FROM JAVIO TO YOU DEAR CUSTOMER

Unaposikia fundi dishi je unaelewa nini? Hapa kidogo tumeshindwa kuelewa nani ni fundi dish na nani ni fundi wa kitufulani. Kuwa makini kila unaponunua dish lako, unaweza kukutana na wajuaji wataokuambia mbona rahisi tu kufunga, usidanganyike dish ni satellite na lazima lifengwe na mtu aliyepitia taaluma ya satellite installation. Tumepata malalamiko mengi kutoka kwa wateja lakini yanakosa tija sababu ya wateja kupenda urahisi wa mambo (bei) mpaka dish linapoteza uelekeo (signal) hapo ndio mtu anakumbuka kumwita fundi aliebobea kwenye taaluma hii. Natoa rai kwako ndugu mteja tambua hili kabla ya matatizo ya kulipa mafundi matapeli na kukufanyia kazi mbovu. Lipa pesa nzuri upate kufanyiwa kazi nzuri itakayo dumu

No comments:

Post a Comment